Kada wa Chadema na mbunge wa zamani wa Arumeru Magharibi, Goodluck Ole Medeye ametangaza leo rasmi kuhamia chama cha UDP.
Ole Medeye amezungumza hayo mbele ya mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi za Makao Makuu ya chama hicho,Mwananyamala jijini Dar.
Medeye amezungumza kwa kujipambanua kuwa yeye anasimamia haki na demokrasia, na kwamba amekerwa sana na tabia ya vyama vya Upinzani kutomheshimu Naibu Spika,Dkt. Tulia Ackson Mwansasu,pichani kati ni Mwenyekiti wa chama cha UDP,Mh.John Cheyo akishuhudia tukio hilo.
Ole Madeye ambaye amehamia chama hicho ikiwa ni baada ya miezi tisa tangu alivyojiunga na Chadema akitokea CCM Agosti 2015, amekabidhiwa kadi ya UDP na Mwenyekiti wa chama hicho, John Cheyo akiwa na wafuasi wengine tisa wapya kutoka Chadema akiwamo mke wake, Anatonia Lekule.
Post a Comment