Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

RAIS MAGUFULI AFUTURISHA TENA IKULU


Raiswa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais Dkt. Magufuli amefuturisha makundi mbalimbali ikiwemo viongozi wa dini, chama Serikali ya mkoa, Watoto Yatima na wenye ulemavu wa ngozi Albino, Wavuvi wa ferry, walemavu vya viungo pamoja na wafanyakazi wa Ikulu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir wakati wakielekea kufuturu Ikulu jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda na Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Alhadi Mussa Salum. 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir mara baada ya kufuturu na makundi ya watu mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na makundi mbalimbali (hawapo pichani)ikiwemo viongozi wa dini, chama Serikali ya mkoa, Watoto Yatima na wenye ulemavu wa ngozi (Albino),walemavu wa viungo pamoja na wafanyakazi wa Ikulu mara baada ya kuwafuturisha Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir , Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Alhadi Mussa Salum pamoja Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda wakiwa wamesimama wakati wa dua mara baada ya kufuturu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa kwenye foleni ya kupata futari pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda Ikulu jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wananchi wakifatilia kwa makini hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza mtoto mwenye ulemavu wa ngozi aliyetambulika kwa jina moja la Yusuph mara baada ya kuwafuturisha Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na baadhi ya makundi ya akina mama waliojumuika katika futari hiyo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na baadhi ya watoto wenye ulemavu wa ngozi (Albino) mara baada ya kuwafuturisha Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rev Vernon Fernandes wa kanisa la Agape mara baada ya kufuturu pamoja na makundi mbalimbali ya wananchi Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir mara baada ya kumaliza tukio la kufuturisha makundi hayo Ikulu jijini Dar es Salam. PICHA NA IKULU
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top