Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

RC MAKALA KIBOKO ... ATENGUA AMRI YA JIJI YA KUVIFUNGIA VIWANDA VIDOGO 28

 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akiangalia ukoboaji mpunga katika mashine moja katika eneo viwanda vidogo eneo la Sido jijini  Mbeya

 Wanancnhi wakimngoja mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla ili kutatua changamoto ya  ukoboaji mpunga  katika eneo viwanda vidogo eneo la Sido jijini  Mbeya

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akkwasili kutatua changamoto ya  ukoboaji mpunga  katika eneo viwanda vidogo eneo la Sido  jijini  la Mbeya

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla ametengua AMRI ya kuvifungia viwanda vidogo 28 vya kukoboa mpunga eneo la Sido iliyotolewa na jiji la Mbeya kupitia idara ya mazingira sababu ya kuvifungia viwanda hivyo zikielezwa kuwa ni mlundikano wa pumba katika maeneo hayo

Uamuzi wa kutengua amri hiyo ametoa leo kwenye ziara ya kutembelea ofisi ya Sido  Mkoa na kisha kutembelea karakana ya sido, viwanda vidogo vya uzindikaji na ukamuaji mafuta ya alizeti na viwanda vya kukoboa mipunga eneo la sido na hapo ndipo alipokutana na umati wa wananchi wakiomba msaada wake kwakuwa viwanda hivyo vimebeba ajira ya watu zaidi ya 2000

Baada ya kuwasikiliza wananchi hao alitangaza kutengua amri hiyo kwa kuwa kuvifunga viwanda hivyo kutafanya mchele kuadimika na bei itapanda na si jambo jema hasa kipindi hiki cha mfungo wa mwezi mtukufu
Pili ametengua amri hiyo ikizingatia kuna ajira zaidi ya watu 2000 .

 "Kwa amri hii ya kufunga ukoboaji hivi Hawa watu 2000 wanakwenda wapi? Kama si kurudi mtaani na kwa vijana ni hatari. Hii kauli ya hapa kazi tu kwa Hawa watu 2000 wataifanyia wapi?"
Ameagiza Mkuu wa wilaya, jiji , jumuiya ya wakoboaji washirikiane na uongozi wa Mbeya cement ambao ndiyo watumiaji wa pumba hizo kuongeza uwezo wa kusomba pumba hizo
Akiwa eneo la Sido magari ya Mbeya cement yaliendelea kusomba pumba na wamemuhaidi Mkuu wa mkoa ndani ya wiki mbili pumba zote zitakuwa zimesombwa
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top