Serikali imekanusha madai ya kuwepo kwa taarifa ya kuwa haina mpango wa kuwapanga vijana waliohitimu kidato cha nne kwenda kidato cha tano kwa sababu mbalimbali.
Akiongea leo Bungeni Mjini Dodoma, Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amesema kuwa taarifa hizo ni za uvumi na serikali kwa sasa ipo katika mchakato wa upangaji wa majina hayo na wakati wowote mwisho mwa mwezi majina yatakuwa yametolewa.
Waziri Mkuu Majaliwa amesema moja ya sababu za kuchelewa kwa matokeo hayo ni pamoja na wizara kubadili mfumo wa GPA, kwenda Division hivyo mchakato huo ndio unafanywa na serikali ili wanafunzi wote wapate madaraja yao na waweze kupangiwa shule.
Mhe. Majaliwa amesema suala la upangaji halikuwa kwa kidato cha tano peke yake bali pia wale wanaokwenda vyuo mbalimbali na kusema kuwa baada ya kukamilika watatoa majibu yao wiki mbili kabla ili wazazi waweze kujiandaa kuwapeleka watoto mashuleni.
Post a Comment