Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

TATIZO LA SUKARI KUMALIZIKA WIKI HII

MKUU wa Mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda amesema kuanzia wiki ijayo tatizo la sukari litakuwa historia, kwani viwanda vya sukari vya ndani vinaanza uzalishaji.

Ntibenda alisema hayo jijini hapa wakati akikabidhi mradi wa ufugaji kuku wa kienyeji na mbuzi wa maziwa katika Kata ya Muriet eneo la Kwamrombo, unaoendeshwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).

“Hivi sasa wananchi mnauziwa sukari kilo moja kwa shilingi 2,500 hadi Sh 3,500 kwa kilo moja, lakini sasa tunasema sukari itapatikana kuanzia wiki ijayo na wanaofunga Ramadhan wasiwe na shaka, watapata sukari,” alisema.

Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro alisema anaungana na serikali kuhakikisha maendeleo ya jiji la Arusha yanapatikana, ikiwemo ukusanyaji wa kodi za majengo.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top