JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA.
• WATU WAWILI WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUJIHUSISHA NA BIASHARA YA MADAWA YA KULEVYA AINA YA BHANGI WILAYANI ILEMELA NA NYAMAGANA.
KWAMBA MNAMO TAREHE 14.06.2016 MAJIRA YA SAA 10:30HRS KATIKA ENEO LA IGOMBE KATA YA BUGOGWA WILAYA YA ILEMELA MKOA WA MWANZA, ASKARI WAKIWA KWENYE DORIA NA MISAKO WALIFANIKIWA KUMKAMATA JONATHAN GABRIEL MIAKA [31] MKAZI WA BUGOGWA AKIWA NA MISOKOTO MIA NNE [400] YA BHANGI KITENDO AMBACHO NI KINYUME NA SHERIA ZA NCHI.
INADAIWA KUWA MTUHUMIWA ANAFANYA BIASHARA YA KUUZA MADAWA HAYO YA KULEVYA KATIKA MITAA MBALIMBALI YA IGOMBE NA ILEMELA PIA, NA PINDI MTUHUMIWA ANAKAMATWA ALIKUWA AKIFANYA MAWASILIANO NA WATEJA WAKE JINSI YA KUWAPATIA BHANGI HIYO.
KATIKA TUKIO LINGINE LA TAREHE TAJWA HAPO JUU MAJIRA YA SAA 13:30HRS KATIKA ENEO LA MWANANCHI WILAYANI NYAMAGANA, ASKARI WAKIWA DORIA WALIFANIKIWA KUMKAMATA RAMADHANI HAMAD MIAKA [24] MKAZI WA NYAKATO AKIWA NA BHANGI KILO TATU [03] KITENDO AMBACHO NI UVUNJWAJI WA SHERIA NA TARATIBU ZA NCHI.
AIDHA INASEMEKANA KUWA MTUHUMIWA AKISHIRIKIANA NA WENZAKE HUFANYA BIASHARA YA KUUZA BHANGI KATIKA MITAA HIYO WANAYOISHI, NDIPO RAIA WEMA WALITOA TAARIFA POLISI NA KUFANIKIWA KUMKAMATA MTUHUMIWA AKIWA NA KILO HIZO ZA BHANGI.
WATUHUMIWA WOTE WAWILI WAPO CHINI YA ULINZI WA JESHI LA POLISI, HUKU MAHOJIANO DHIDI YA UHALIFU WANAOUFANYA WA KUJIHUSISHA NA BIASHARA YA BHANGI UKIENDELEA, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA WATUHUMIWA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI KUJIBU MASHITAKA YANAYO WAKABILI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI HASWA VIJANA AKIWATAKA KUACHA KUJIHUSISHA NA BIASHARA ZA MADAWA YA KULEVYA AMBAYO NI HARAMU NA BATILI KATIKA USTAWI WA NCHI YETU, KWANI JESHI LA POLISI LIMEJIPANGA VIZURI KUHAKIKISHA LINAWATAFUTA WALE WOTE WANAOJIHUSISHA KATIKA BIASHARA HIYO NA KUWAKAMATA KISHA KUWAFIKISHA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA KWA AJILI YA KUPEWA ADHABU KALI ILI IWE FUNDISHO KWA WATU WENGINE.
IMESAINIWA NA:
SACP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA.
Post a Comment