Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-WAZALENDO), Zitto Kabwe (kulia) akitoka katika kituo kikuu cha polisi jijini Dar es Salaam baada ya mahojiano.
MBUNGE wa Kigoma Mjini ambaye pia ni Kiongozi Mkuu chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, mapema leo aliitikia wito kutoka kwa Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Camilius Wambura, wa kufika katika kituo kikuu cha polisi polisi jijini Dar alipohojiwa kwa zaidi ya saa tatu.
Akizungumza na wanahabari kituoni hapo mara baada ya kutoka, mwanasheria wake, Stephan Mwakibola, alisema kuwa kiongozi huyo amehojiwa kuhusiana na maudhui ya hotuba ambayo aliitoa Jumapili iliyopita katika mkutano uliofanyika katika Viwanja vya Mbagala- Zakhem jijini Dar.
Naye Zitto alisema kuwa anasikitika kuona siku hizi kiongozi wa chama cha siasa anapokwenda kwenye mikutano analazimika afikirie kutafuta maneno ya kuzungumza.
Mwakibola alieleza kuwa polisi wamemruhusu Zitto kuendelea na shughuli zake za kila siku baada ya kupewa dhamana, na Jumatano ijayo ametakiwa kuripoti tena polisi. Hata hivyo, wakili huyo hakuwa tayari kuweka bayana sehemu ya hotuba ambayo ililileta utata kwa sababu suala hilo bado liko chini ya upelelezi.
NA DENIS MTIMA/GPL
Post a Comment