Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa Ikishirikiana na Jeshi la Polisi pamoja na Takukuru iliyopewa jukumu la kuchunguza Mradi wa jengo la Biashara la machinga Complex la jijini ambalo limebaini Ubadhilifu mkubwa wa fedha za Ujenzi wa jengo hilo,Mkataba wenye utata pamoja na malimbikizo ya riba ambayo inaongezeka kila kukicha kinyume cha utaratibu.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa mkoa wa dsm Paul makonda ambaye alikabidhiwa usimamizi wa jengo hilo na waziri wa Nchi Ofisi ya rais Tamisemi George Simbachawene april 19 Mwaka huu baada ya kuvunja bodi kutokana na jengo hilo kuendeshwa kwa hasara amesema mkataba unaonyesha kuwa Gharama ya jengo hilo ilikuwa million 12 .7 lakini mara tu baada ya kukabidhi kwa jiji jengo hilo Nssf Ilikuwa inalidai jiji bilion 7.
Aidha amesema jengo hilo lilitakiwa kuwa na Vyuma 10,000 lakini hivi sasa kuna vyumba 42,000\= huku vyumba vingine havijulikani vilipo huku kila upande ukipungua Ghorofa Moja moja tofauti na mkataba wa ujenzi wa jengo hilo.
Kutokana na kadhia hiyo Mkuu wa mkoa amependekeza hatua kadhaa zichukuliwe na waziri Simbachawene kutokana na deni kubwa la Shilingi billion 38.7 Huku jengo hilo tangu lifunguliwe likiwa limelipa milion mia tano tu,huku wahusika wote wa Nssf na Halmashauri ya jiji kuchukuliwa hatua ili fedha hizo zirejeshwe.
Loading...
BLOG RAFIKI
-
-
-
-
-
-
Jioni12 hours ago
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
Post a Comment