Dar es Salaam. Safari ya mashindano ya Ndondo Cup iliyoanza miezi mitatu iliyopita, inafikia tamati leo kwa mchezo wa fainali kati ya Kauzu FC dhidi ya Temeke Market.
Mchezo wa leo unaotarajia kuwa na ushindani wa aina yake utapigwa kwenye Uwanja wa Bandari uliopo Temeke na unatarajiwa kuvuta mashabiki wengi wa soka jijini Dar es Salaam.
Gazeti la Mwanaspoti ambalo ni miongoni mwa wadhamini wa mashindano hayo limeahidi kuwaletea habari motomoto kupitia jarida maalumu kwa ajili ya mashindano hayo.
Mwandishi mwandamizi wa gazeti hilo linalochapishwa na Kampuni ya Mwananchi Communication Limited, Badru Kimwaga amesema jarida la leo litakuwa na mjumuiko wa matukio yaliyojiri katika mashindano hayo.
Loading...
Post a Comment