File Photo
Ajali hiyo imetokea wakati wataalamu hao wakiwa kazini kusimamia ujenzi wa barabara. Dereva wa gari lililokuwa limewabeba, Juma Nassoro alijeruhiwa na kupelekwa Hospitali ya Wilaya ya Korogwe, Magunga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba amesema ajali hiyo ilitokea juzi saa tano asubuhi katika Kijiji cha Makwei, Kata ya Vugiri, Tarafa ya Bungu.
Wakulyamba amewataja waliokufa kuwa ni Eliapenda Edward (33) ambaye ni Mhandisi wa Tanroad, Noel Madola (22) na Twaha Chande (49) waendesha mitambo wa mkandarasi anayejenga barabara hiyo.
Post a Comment