KATIBU Mkuu wa Baraza la Vijana wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha) Julius Mwita amekamatwa na Jeshi la Polisi mchana huu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.
Mwita na vijana wengine watatu ambao hawakufahamika majina yao mara moja wamekamatwa kwa sababu ambazo hazijafahamika mpaka sasa wakati wakisubiri Tundu Lissu Mwanasheria Mkuu wa Chadema kufikishwa mahakamani hapo.
Mwandishi ameshuhudia Mwita na vijana wawili wakikamatwa ndani ya eneo la mahakama na kuingizwa ndani ya gari ya polisi yenye namba za usajili PT 1848.
Kijana mwingine mmoja amekamatwa akiwa nje ya uzio wa mahakama hiyo ambapo askari waliojihami kwa silaha za moto wameimarisha ulinzi ndani na nje ya mahakama ya Kisut.
Vijana wote wanne tayari wameondolewa mahakamni hapo na gari ya polisi ambapo inaaminika kuwa watapelekwa Kituo Kikuu cha Polisi, Dar es salaam kwaajili ya mahojiano.
Post a Comment