Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

SHIBUDA AIBUKIA MKUTANO WA RAIS MAGUFULI JIJINI MWANZA


Katibu Mkuu wa Chama cha ADA-Tadea, John Shibuda jana alijitokeza katika mkutano wa Rais Dkt. John Magufuli katika viwanja vya Furahisha Jijini Mwanza na kumpongeza Rais Dkt. John Magufuli kwa namna ambavyo anatatua kero za wananchi.

Akihutubia maelfu ya wakazi wa Mwanza na maeneo jirani waliojitokeza kumsikiliza Rais Dkt. Magufuli , Shibuda alivitaka vyama vingine vya siasa nchini kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kuwa kazi anayoifanya ni kwa ajili ya watanzania wote.

"Mheshimiwa Rais Magufuli endelea kuwahudumia watanzania na nikuambie sijawahi kuona mchongoma unang’olewa kwa upepo au sijawahi kuona utelezi wa mlenda unamwangusha mtu mzima" - Alisema Shibuda.

Shibuda alisema vyama vya UKAWA vinapaswa kutambua kwamba Rais Dkt. Magufuli ni mtu mzuri ndiyo maana aliwasaidia kumaliza mgogoro wa uchaguzi wa Meya Jijini Dar es Salaam hivyo watambue mchango wake kwa taifa .

Aidha Shibuda alimuomba Rais  Magufuli kwamba akipata muda aende akamweleze vizuri matatizo yanayowakabili wakulima nchini.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top