Chama cha wananchi CUF kimekutana na waandishi wa habari Dodoma na kumtaka msajili wa vyama vya siasa nchini asitumike kukiyumbisha chama hicho kwa madai baadhi ya vyama vinatumia ofisi yakekuwavua uanachama ikiwa ni pamoja na madai ya aliyekuwa mwenyekiti wao Profesa Ibrahim Lipumba kutaka kutaka kurudi katiaka nafasi hiyo.
Mwenyekiti wa CUF bungeni Riziki Mngwali amesema…’Baraza kuu CUF liliwavua uanachama wanachama kadhaa akiwemo Prof Lipumba na kuwaandikia barua, tunaunga mkono hatua hiyo ya kinidhamu‘
‘Lakini pia tuna taarifa za Prof Lipumba kupeleka malalamiko yake kwa msajili wa vyama vya siasa akijitangaza kuwa yeye ni M/kiti halali wa CUF‘ –Riziki Mngwali
‘Ifahamike kuwa sisi CUF hatumtambui Prof Lipumba kuwa M/kiti wetu na kwasasa chama kinaongozwa na chama taifa chini ya Julius Mtatiro‘ –Riziki Mngwali
Post a Comment