Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Idadi ya watu wanaofariki kwa tetemeko la ardhi yazidi kuogezeka

Serikali imeliambia Bunge kuwa idadi ya vifo vilivyotokana na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera imeongezeka na kufikia 17 huku watu 169 bado wamelazwa na imetuma madaktari bingwa 15 kutoka mkoani Mwanza kwenda kuimarisha utoaji wa tiba kwa waathirika wa tukio hilo.

Waziri wa nchi ofisi ya rais –Tamisemi Mhe.George Simbachawene amesema katika tukio hilo watu 83 wamepatiwa tiba na kuruhusiwa kurejea majumbani huku nyumba 840 zikianguka na zingine 1884 zikipata nyufa yakiwemo majengo 44 ya Serikali.

Mara baada ya kauli hiyo ya Serikali bungeni, Mbunge wa Jimbo la Mhe.Rashid Shangazi aliwasilisha hoja bungeni hapo kuliomba bunge lijadili suala hilo kwa nusu saa ambapo wabunge wote kwa kauli moja walikubaliana juu ya hilo na kuitaka Serikali ifanye haraka zoezi la utathmini wa uharibifu uliojitokeza sambamba na kuwahudumia waathirika wa tukio hilo.

Serikali imewahakikishia wabunge hao kuwa inalichukulia tukio hilo kwa uzito wa pekee na kwamba mpaka muda huu linashughulikiwa na Serikali hiyo chini ya usimamizi wa moja kwa moja wa Waziri Mkuu Mhe.Khasim Majaliwa.

Mhe.Willium Lukuvi-Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Mara baada ya hayo bunge liliendelea na shughuli zake za kawaida ambapo wabunge waliendelea kuijadili miswada ya sheria ya mamlaka ya maabara ya mkemia mkuu wa Serikali na ule wa baraza la wanataaluma wa kemia yote ya mwaka 2016.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top