Loading...
IGP Ernest Mangu 'alamba ulaji' mpya
Wakuu wa majeshi ya polisi katika nchi za Afrika zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara (SADC), wanatarajiwa kumpa uenyekiti wa Shirikisho la Majeshi ya Polisi Kusini mwa Afrika (Sarpcco), Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP), Ernest Mangu.
Msemaji wa jeshi hilo nchini, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Advera Bulimba alisema jana kuwa IGP Mangu atashika nafasi hiyo kwa mwaka mmoja. Mangu anapokea kiti hicho kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Msumbiji.
Chanzo: mwananchi.
Post a Comment