SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imewasilisha marekebisho ya Katiba ya Zanzibar ya 11 ya mwaka 1984, ambayo yatatoa nafasi na kumpa uwezo Rais wa Zanzibar, kuchagua wajumbe wa Baraza la Wawakilishi bila ya kushauriana na Kiongozi wa Upinzani ambaye kwa sasa hayupo katika baraza hilo.
Kwa mujibu wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Haroun Ali Suleiman, katika marekebisho hayo vifungu viwili vinahitaji kufanyiwa marekebisho kikiwemo cha 66 kwa kufanya marekebisho na kufuta maneno ya vyama na kiongozi wa upinzani.
Akifafanua katika kifungu hicho, alisema lengo lake ni kutoa nafasi kwa Rais wa Zanzibar kuchagua nafasi mbili za wajumbe wa Baraza la Wawakilishi bila ya kushauriana na Kiongozi wa Upinzani katika Baraza ambaye kwa sasa hayupo, baada ya Chama cha Wananchi (CUF) kususia Uchaguzi Mkuu wa marudio mwaka huu, na hivyo kutopata mwakilishi yeyote na hivyo kufutika kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ambayo Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad alikuwa Makamu wa Kwanza wa Rais.
Haroun alisema katika mazingira ya sasa katika Baraza la Wawakilishi, hakuna kiongozi katika Baraza hilo pamoja na vyama vilivyopata wingi wa kura, hatua ambayo imemfanya Rais kushindwa kuteua wajumbe wawili katika Baraza la Wawakilishi.
‘Katika Baraza la Wawakilishi la sasa Rais ameshindwa kuteua wajumbe wawili katika nafasi kumi ambapo anatakiwa ashauriane na kiongozi wa upinzani ambaye hayupo kwa sasa,” alifafanua na kuongeza kuwa Kifungu cha 77(2) kinafuta neno la upinzani lenye uwakilishi ndani ya Baraza la Wawakilishi.
Akifafanua, alisema marekebisho ya Katiba yanayopendekezwa mbele ya Baraza la Wawakilishi, lengo lake kubwa kuimarisha demokrasia na kumpa nafasi Rais kuchagua wajumbe wa Baraza watakaofanya kazi kwa maslahi ya taifa. Katiba ya Zanzibar imempa mamlaka Rais wa Zanzibar kuchagua wajumbe 10 katika Baraza la Wawakilishi, ambapo nafasi mbili kwa kushauriana na kiongozi wa upinzani ambaye hayupo kwa sasa.
Wajumbe watatu wa Baraza la Wawakilishi walioteuliwa kutoka katika vyama vya upinzani, wanatokana na nafasi 10 kwa mujibu wa uwezo aliopewa Rais na Katiba. Wajumbe hao watatu kutoka vyama vya upinzani ni Hamad Rashid Mohamed, Juma Ally Khatib na Said Soud Said.
Loading...
BLOG RAFIKI
-
-
-
-
Duniani Leo1 hour ago
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
Post a Comment