KAHAMA: Sataka la kuhamisha makao makuu ya Halmashauri ya Msalala kuyatoa kata ya Busangi na kuyapeleka Ntobo bado ni kitendawili kikubwa baada ya waziri wa zamani wa serikali ya awamu ya nne wa wizara ya maliasili na utalii Ezekiel Maige kuleta taflani kwenye mkutano wake uliofanyika Kata ya Busangi
Katika Mkutano huo ambao aliufanya kama mbunge wa Jimbo hilo la Msalala wananchi wa kata ya Busangi waliususia mkutano wake baada ya kuwaeleza kuwa hakuna namna maazimio yalilshapitishwa na baraza la madiwani wa Halmashauri ya Msalala kuyatoa Busangi makao hayo na kuyapeleka Ntobo
Wananchi hao waliamua kuondoka kwenye mkutano wa mbunge huyo baada ya kuelezwa hivyo huku wakidai kwamba vitendo vya rushwa vilishamiri katika suala hilo kwani walikuwa hawatarajii uamuzi huo wa kuhamisha makao hayo ambayo tayari yanatambulika mpaka Wizara ya Tamisemi
Kabla ya mkutano huo wa Mbunge kwenye kata hiyo ya Busangi takribani miaka 3 kumekuwa na mvutano mkubwa wa kuhamisha makao hayo ambapo awali makao hayo yalihamishwa Busangi na kupelekwa Segese na baadae pia kuhamishwa hapo na kupelekwa Mega na baadae tena kuhamishwa hapo na kupelekwa Ntobo
Mkazi wa kata hiyo Julius Katto alisimama na kuuliza swali kwa mbunge kuwa maadhimio ya baraza la madiwani ya kujengwa kwa makao makuu ya wilaya hiyo ni wapi maana kumekuwa na sintofahamu kati ya Busangi na kata ya Ntobo kijiji cha Mega hali ambayo inawachanganya wananchi .
“Mbunge wewe ni muwakilishi wetu ulitetea kuleta kuwa wilaya na makao makuu yakapendekezwa Busangi na yakapitishwa na Waziri mkuu sasa ni nini kilichofanyika kuyabadilisha makao hayo kuyaondoa hapa na kuyapeleka huko” aliuliza Katto
Vicent Magembe ambaye pia aliuliza swali kwa mbunge Maige kuwa itakuwaje makao makuu kujengwa kata ya ntobo na sio busangi ambapo waziri mkuu wa awamu iliyopita mizengo pinda alisema makao makuu ya wilaya hiyo yajengwe busangi na barua ipo inayoonyesha kupitishwa kwa makao hayo kujengwa Busangi lakini barua ya Waziri mkuu kuonyesha kujengwa makao hayo Ntobo haipo.
Akijibu maswali hayo mh.Maige alisema wananchi wanatakiwa kutoa mapendekezo ni sehemu ipi sahihi lakini serikali iliamua kuweka makao makuu yake katika kata ya Ntobo hivyo yeye hana mamlaka ya kupinga maadhimio ya serikali japo ikiwa ni mmoja wa viongozi wa ngazi ya juu katika Halmashauri hiyo.
Majibu hayo ndiyo ikawa mwisho wa mkutano huo baada ya wananchi hao waliojitokeza walianza kusimama na kuanza kuondoka wakidai kuwa mbunge wao aliamua kuwatelekeza kwa makusudi kwani alikuwa akihudhuria vikao vya madiwani juu ya sakata hilo la makao makuu na wakati wanahamisha alihudhuria lakini ameshindwa kutoa majibu ya kuridhisha
Loading...
Post a Comment