RAIS John Magufuli ametoa zawadi za vyakula vya thamani ya Sh milioni 6.4 kwa vituo 14 vya watoto wanaoishi katika mazingira magumu, yatima, walemavu na wazee kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya Idd el Haj, kesho.
Zawadi hizo zilikabidhiwa kwa walezi wa vituo hivyo jana Dar es Salaam na Kaimu Kamishna Msaidizi wa Ustawi wa Jamii, Rabikira Mushi na kueleza kuwa Rais Magufuli ameona umuhimu wa kushiriki kusherehekea pamoja na makundi hayo katika jamii.
Alisema zawadi hizo zinatolewa kwa vituo vinne vilivyoko Dar es Salaam, viwili vya Zanzibar na vituo vinane katika mikoa mingine ya Tanzania Bara.
Alivitaja vituo vitakavyopata zawadi hizo kuwa ni makao ya Taifa ya watoto yatima Kurasini, mahabusu ya watoto yaliyoko Upanga, kijiji cha furaha Arch Diocese of Dar es Salaam na Dar al arqum, International Islamic Relief Organization.
Vituo vingine ni kituo cha Mabaoni Chakechake Pemba, makazi ya wazee na wasiojiweza Sebleni-Unguja, shule ya maadilisho Irambo Mbeya.
Yamo makazi ya wazee ya Bukumbi, Misungwi, Mwanza, ya Sukamahela, Manyoni, Singida na ya Kibirizi, Kigoma. Mushi alivitaja vituo vingine kuwa ni makazi ya wazee ya Nyabange, Musoma, Mara, Chazi, Morogoro, Ngehe, Ruvuma na ya Nandanga Masasi.
Mushi alisema Rais Magufuli ameangalia watoto na wote walio katika mazingira magumu na kwamba amefanya kadri awezavyo na jamii iwakumbuke zaidi na kujitokeza kuwasaidia watoto hao.
Akipokea zawadi, mlezi wa kituo cha makao ya taifa ya watoto yatima, Kurasini, Zuwena Mziray alisema watoto wamefurahi kwa zawadi hizo kwani zitawawezesha kufurahi sikukuu hiyo kama walivyo watoto wengine.
Kuhusu matatizo yanayowakabili watoto waishio katika mazingira magumu, alisema ni pamoja na watoto kutopata mahitaji yao kama inavyostahili na kuisihi jamii kuwa na tabia ya kuwatembelea na kuwapa misaada mbalimba
Loading...
BLOG RAFIKI
-
-
-
Athari za ugonjwa wa tezi dume3 hours ago
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
Post a Comment