Loading...
SERIKALI YATOA KAULI BUNGENI KUHUSU TETEMEKO LA ARDHI KAGERA
#Serikali yatoa msaada kwa waathirika kwa kuwapatia makazi ya muda baadhi ya wananchi ambao nyumba zao zimeathirika kwa majirani.
#Serikali imeelekeza wanajiolojia kutoa maelekezo ya kisayansi ili kuwatoa hofu wananchi kuhusu hali hiyo.
# Serikali imeongeza nguvu ya madaktari bingwa 15 toka mkoani Mwanza ili waweze kutoa huduma haraka kwa waathirika.
#Serikali imewahamasisha pia wananchi waweze kusaidiana pale inapowezekana.
#Serikali imewaagiza Wakurugenzi Manispaa ya Bukoba na Halmashauri ya Bukoba kufunga kwa mudw Shule za Ihundo Sekondari na Nyakato Sekondari kwa kuwa zina hali mbaya.
#Serikali inaendelea kuhakikisha hatua za dharura zinachukuliwa kwa kushirikiana na wadau wengine kuhakikisha kuwa hatua za muda mfupi na muda mrefu zinatambuliwa na kutekelezwa ili kuwasaidia wahanga.
# Serikali inaendelea kufanya tathimini ya athari zilizosababishwa na tetemeko la ardhi.
# Serikali inaomba wadau wote wa Ndani na Nje wanaotaka kuchangia wawasiliane na *Ofisi ya Waziri Mkuu na Kamati ya Maafa ya Mkoa tu*.
#Serikali inatoa onyo kwa yeyote mwenye kutumia maafa haya kama sehemu ya kujinufaisha.
#Serikali imewataka wananchi kuwa wavulimivu na kuendelea kushirikiana na Serikali katika kutatua tatizo ambalo limeipata nchi ili wananchi waendelee kupata huduma kulingana na athari za tetemeko.
#Waheshimiwa wabunge wameunga mkono juhudi hizo za Serikali na wameridhia kwa kauli moja kukatwa posho yao ya siku moja ili kuchangia maafa hayo.
*Imetolewa na Idara ya Habari-MAELEZO*
Post a Comment