Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameahirisha ziara yake ya siku tatu Nchini Zambia ambapo pamoja na mambo mengine ilikuwa ahudhurie Sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Sita wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu, ili aweze kushughulikia tatizo laTetemeko la ardhi lililosababisha vifo vya watu 16, mamia wakiwa wamejeruhiwa na nyumba kadhaa zimebomoka Mkoania Kagera
Kufuatia kuahirishwa kwa ziara hiyo Mheshimiwa Rais Dkt.Magufuli amemtuma Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Kumuwakilisha katika Sherehe hizo za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Sita wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu
Sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Sita wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu zinatarajiwa kufanyika kesho tarehe 13 Septemba, 2016 katika jiji la Lusaka
Jaffar Haniu
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi
Dar es salaam
Post a Comment