Meya wa Mnaispaa ya Kinondoni Boniface Jakob
Uamuzi huo unatokana na Serikali kutangaza wilaya mpya za Ubungo na Kigamboni hatua itakayoifanya Dar es Salam kuwa na wilaya tano kutoka tatu za awali.
Meya wa Kinondoni, Boniface Jacob amesema uamuzi huo umefikiwa katika kikao cha Baraza la Madiwani usiku huu.
Amesema kabla ya uamuzi huo, vikao mbalimbali vya kiutendaji vilifanyika ambavyo pia vilizungumzia mgawanyo wa rasirimali pamoja na watumishi.
"Baada ya siku 14 tunatarajia wakurugenzi wa Manispaa za Kinondoni na Ubungo wataitisha uchaguzi wa kumpata Meya na Naibu meya," alisema Jacob.
Kwa mujibu wa Jacob, Kinondoni itabaki na kata 20 wakati Ubungo itakuwa na kata 14.
Post a Comment