Afande Sele akiwa na Kiongozi wa ACT, Zitto Kabwe, kabla ya uchaguzi mkuu wa 2015.
Msanii mkongwe wa muziki kutoka mkoani Morogoro, Afande Sele ambaye alikuwa mgombea nafasi ya ubunge katika uchaguzi uliopita kwa tiketi ya ACT Wazalendo amefunguka kwa kuonyesha kutoridhishwa na mwenendo wa viongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo.
Rapper huyo amesema viongozi wa chama chake hawaeleweki wapo upande gani kutokana na kubadilisha misimamo yao kila mara.
“Chama changu cha Act-Wazalendo bwana wakati flani hata mimi sikielewi kama ni malaika au shetani. Ni kama kiumbe aitwae mkunga haeleweki ni samaki au nyoka zaidi tumekuwa kama popo hatupo katika kundi la ndege au mnyama…labda hatueleweki au hatujielewi kwa mfano wakati wa kampeni viongozi wetu walijikita kuponda wapinzani wenzetu hasa mzee Lowasa na UKAWA na baada ya uchaguzi viongozi wetu wakampongeza Magufuli kiasi cha kujipendekeza hadi wakampa Ilani ya chama chetu akaitumie akiwa Ikulu. sasa ajabu leo hii tumegeuka tena kwa kiongozi mkuu kila siku anamponda Rais Magufuli na chama chake halafu kiongozi wangu mwingine comrade mchange yeye kila siku anamponda mzee Lowasa na ukawa yake” aliandika kupitia facebook.
Aliongeza “Katika mgogoro wa CUF unaoendelea sasa hivi eti viongozi wote hao wa chama chetu wamejigeuza team Lipumba…sasa sielewi sisi kama wanachama tusimamie wapi….’Nyuma ya pazia’dilidilisha…mchongo=mchongoma…ni bora kuwa Moto au Baridi kuliko kuwa vuguvugu kwani vuguvugu ni ishara ya unafki ambao hata maandiko yanakataza…Kweli itatuweka huru,”
Loading...
BLOG RAFIKI
-
-
-
Wafungwa watoroka gerezani DRC1 hour ago
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
Post a Comment