Nyumba namba 34 iliyojengwa katika kitalu (block) namba 2 iliyopo Bunju B mtaa wa kihonze maarufu kwa Ferous, wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es salaam inayomilikiwa na aliyekuwa mbunge wa Kisesa na mkurugenzi wa uenezi wa muda mrefu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, BwanaERASTO TUMBO, kesho jumapili tarehe 2.10.2016 saa nne asubuhi inapigwa mnada kufidia deni la milioni 300 alilokopa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Tanzania Bara John Mnyika ambaye pia ni Mbunge wa Kibamba kuwakilisha chama hicho, Jamvi la Habari limeelezwa.
Moja ya Nyumba iliyomdhamini Mnyika kukopa.
Taarifa za uhakika ambazo Jamvi la Habari linazo zinasema kuwa tayari mawakala wa kukusanya madeni wa Benki aliyokopa mnyika (Tunaihifadhi) kiasi hicho cha fedha wameshapita kutangaza matangazo ya kuhusu mnada huo na kwamba kesho saa nne asubuhi mnada utapigwa ili kufidia deni hilo ambalo ni sehemu ya madeni mengi yanayomkabili mwanasiasa huyo kijana yanayosemekana kumsababishia msongo mkubwa wa mawazo kiasi cha kushindwa kutimiza wajibu wake ipasavyo.Erasto Tumbo Mdhamini wa moja ya mikopo anayodaiwa Mnyika.
Akizungumza na mwandishi wetu maalum, mmoja wa viongozi wa kampuni ya udalali ya kukusanya madeni na minada walopewa kazi ya kukusanya deni hilo amesema kila kitu kimekamilika na sasa kilichobaki ni kesho kupigwa mnada tu kwa nyumba hiyo
‘’kama una mteja au wewe mwenyewe ni mteja tafadhali karibu sana, kila kitu kimekaa sawa, tumemvumilia sana Mnyika na wenzake, tumesumbuana naye sana Mahakamani, lakini sasa hatimaye kesho tunapiga mnada’’. Alisema
Nyumba hiyo inayomilikiwa na Tumbo, ilitumika kama Dhamana ili imuwezeshe Mnyika kukopa pesa zaidi ya milioni mia tatu katika benki moja maarufu hapa nchini na kwamba Tumbo alimdhamini mnyika kwa kuwa ni kiongozi wake katika chadema na hivyo hakutegemea kama asingeweza kutokulipa mkopo huo ambao hata hivyo inasemekana mnyika na wenzake hawakuwekeza pesa hizo kwenye biashara na badala yake kuwekeza kwenye masuala mengine yasiyohusiana na sababu ya mkopo.
Alipoulizwa na Jamvi la Habari kuwa inakuwaje wapige mnada nyumba ya mtu ambaye hajanufaika na mkopo huo na wasitafute mali nyingine za Mnyika alijibu ifuatavyo ‘’Sisi tunafuata makubaliano ya Mkopo kati ya Mnyika na wenzake dhidi ya benki, na katika mkopo huu dhamana waliyoweka ilikuwa ni nyumba na kwamba mmiliki wake alisaini kukubaliana na matakwa ya kimkataba ikiwemo hili la dhamana kutumika kufidia, sasa aliowadhamini wameshindwa kulipa hakuna jinsi zaidi ya kupigwa mnada tu’’. Alisema
Uchunguzi uliofanywa na Jamvi La Habari unaonyesha kwamba Mnyika kwa sasa hana tena uwezo wa kulipa deni hilo wala mengine yanayomkabili yanayokadiliwa kukaribia kufikia bilioni 1 na kwamba kila anapoulizwa na wadhamini wake huishia kujibu kuwa biashara zimekuwa ngumu na kwamba ana madeni mengi hivyo kwa sasa amekata tama.
Hivi karibuni viongozi wenzake wa CHADEMA akiwemo kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama hicho walilipotiwa kuchangishana kumnusuru mnyika kuingia katika kadhia hiyo ya kufilisiwa.
Taarifa zaidi tutawaletea kesho kabla na baada ya MNADA.
Chanzo: Jamvi la Habari
Post a Comment