Wakati vikao vya Bunge vikianza kesho mjini Dodoma, Chadema imejipanga kukabiliana na hoja za Serikali ukiwamo muswada wa huduma za vyombo habari utakaojadiliwa kabla ya kupitishwa na kuwa sheria.
Katika vikao hivyo, miongoni mwa miswada itakayojadiliwa ni muswada huo na tayari Waziri wa Habari, Nape Nnauye ameshauwasilisha kwenye Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii ambayo imekamilisha kazi yake jana.
Tayari viongozi wa Chadema akiwamo aliyekuwa mgombea urais wa chama hicho mwaka 2015, Edward Lowassa na Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye wametua mjini humo kupanga mikakati pamoja na wabunge wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), jinsi ya kukabiliana na hoja mbalimbali.
Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano, Uenezi na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema alikiri kuwapo kwa vikao kati ya Lowassa na wabunge wa Ukawa, lengo likiwa ni kuukabili muswada huo.
Post a Comment