Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MATUNDA YA RAIS MAGUFULI YAANIKWA



Kitendo cha Rais Magufuli kubana pesa, kubana mianya ya upotevu wa pesa hali inayopelekea pesa kuwa adimu mitaani inazidi kuleta matunda kiuchumi kwa Taifa kutokana na kushuka kwa mfumuko wa bei.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Septemba, 2016 umepungua hadi asilimia 4.5 kutoka asilimia 4.9 ilivyokuwa mwezi Agosti 2016.

Fahirisi za bei zimeongezeka hadi 103.05 mwezi Septemba 2016 kutoka 98.64

Mwezi Septemba 2015 mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi mwezi Septemba 2016 umepungua hadi asilimia 6.0 kutoka asilimia 7.0 ilivyokuwa mwezi Agosti 2016.

Mwenendo wa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula zilizoonesha kupungua ni pamoja na bei za dagaa kwa asilimia 11.6 na viazi vitamu kwa asilimia 3.2.

Kwa upande mwingine mwenendo wa bei za baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilionesha kupungua ni pamoja na bei za gesi kwa asilimia 10.4, dizeli kwa asilimia 2.9 na petrol kwa asilimia 2.8.

Mabadiliko ya bei kati ya mwezi Agosti na Septemba 2016 fahirisi za bei zimepungua hadi 103.o5 mwezi Septemba 2016 kutoka 103.28 mwezi Agosti 2016.

Bidhaa zilizochangia kupungua kwa fahirisi ni pamoja na mchele kwa asilimia 2.6, unga wa mahindi kwa asilimia 1.0, dagaa kwa asilimia 3.0 na mbogamboga kwa asilimia 4.3. Upande mwingine baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kupungua kwa mfumuko wa bei ni pamoja na dizeli kwa asilimia 2.9, petroli kwa asilimia 2.8 na mafuta ya taa kwa asilimia 2.9

Sio hivyo tu hata thamani ya Shilingi yetu imepanda. Thamani ya shilingi ya Tanzania kwa mwezi Septemba 2016 kutoka mwezi Desemba 2015 kuwa na uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia sh.97 na senti 04 mwezi Septemba 2016 kutoka mwezi Desemba 2015 ikilinganishwa na shilingi 96 na senti 83 ilivyokuwa mwezi Agosti 2016.

Magufuli anaiendesha hii nchi kwa mahesabu makali, yale tunayoyaona machungu sasa (kipindi kifupi) yana raha kubwa kwa muda mrefu mbele ya safari.

Nia ya Rais Magufuli ni njema, tuvumilie na tumpe ushirikiano.

*Data kwa hisani ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu*

Shilatu E.J
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top