Mambo yanaendelea kuwa mazito Jangwani kuhusu suala la kuikodisha klabu hiyo kwa kampuni ya Yanga Yetu inayomilikiwa na mwenyekiti wao Yusuf Manji.
Mapema leo Manji alikua na mkutano na wanahabari ambapo aliwasihi wanachama wa Yanga kujitokeza katika mkutano mkuu wa dharura uliopangwa kufanyika Jumapili October 23 katika makao makuu ya klabu.
Lakini taarifa ambayo wapendasoka.com imeipata ni kwamba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imeuzuia mkutano huo baada ya maombi ya wanasheria Frank Chacha na Juma Magoma kukubaliwa.
Kwa mujibu wa nakala za maombi hayo, Frank na Juma wanapinga mchakato wa ukodishwaji wa klabu hiyo kwa kampuni ya Yanga yetu na hivyo wameiomba mahakama izuie mkutano huo kwa sababu ungefanyika wakati ambao shauri lao halijasikilizwa na mahakama.
Japo klabu ya Yanga haijatoa tamko lolote, lakini taaifa tuliyoipata inaonesha maombi hayo yakikubaliwa na hakimu.
Hili huenda likavuruga kabisa hali ya hewa ya klabu ya Yanga ambayo kesho itakua ugenini huko Kagera dhidi ya Kagera Sugar
Post a Comment