BAADHI ya wananchi wa maeneo yanayopita miundombinu ya mafuta na gesi iliyopo kwenye mitambo ya kuzalisha umeme ya Kinyerezi I na mingine inayoendelea kujengwa, wameanza kuhujumu miundombinu hiyo kwa kufanya uharibifu wa aina mbalimbali.
Uharibifu huo ni kuchimba mchanga, kuchoma moto, kunyofoa baadhi ya alama za kwenye mabomba ya gesi na kufanya vyuma chakavu na mengineyo.
Kutokana na hujuma hizo ambazo ni hatari na zinaweza kusababisha madhara makubwa kwa uchumi wa nchi, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limelazimika kuwaita watendaji wa maeneo, wenyeviti wa mitaa, viongozi wa dini zote na wale wa ulinzi na usalama katika maeneo hayo kuweka mikakati ya kutokomeza vitendo hivyo.
Viongozi hao walikutana katika ofisi za Tanesco zilizopo katika mitambo ya kuzalisha umeme ya Kinyerezi I, Kaimu Meneja wa Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Kinyerezi 1, Lucas Busunge alisema lengo la kikao hicho ni kuelimisha usalama wa miundombinu hiyo ili viongozi hao wazungumze na wananchi wao.
Akiwasilisha mada, Ofisa Usalama Mwandamizi wa Tanesco, Misana Gamba alisema kumekuwa na vitendo vinavyotishia usalama wa miundombinu hiyo, ikiwemo kuchimba michanga na kujenga wakati kuna mabomba ya gesi yanayopita chini.
“Tunajiandaa kujenga uzio katika eneo lote la miundombinu hiyo huku wakihakikisha jeshi la polisi na walinzi wake ambao ni jeshi la kujenga taifa wakizungukia katika eneo linalopita miundombinu hiyo wakati wote kuzuia uharibifu,” alisema.
Aliomba viongozi wa mitaa na wananchi kuendelea na ushirikiano katika kulinda miundombinu ya maeneo hayo, kwani toka kituo hicho kuanza kazi kumetokea tukio moja la moto uliowashwa na mtu asiyefahamika ambalo lilidhibitiwa lakini hawakujua sababu yake.
Ofisa Usalama Mkuu wa Shirika la Petroli Tanzania (TPDC), Elias Muganda alisema katika maeneo ambayo mabomba mawili ya gesi yanapita ya Gongo la Mboto katika gereji na Kinyerezi Mwisho, wanapofanyia biashara ni hatari sana.
Alisema tatizo la usalama ni magari makubwa zaidi ya tani saba kupita katika eneo la mkuza wa mabomba ya gesi, wakati kuna vyuma vyenye alama za njano vinavyoonesha bomba la gesi linapita kwa ajili ya usalama vimetolewa na kuuzwa kama vyuma chakavu.
“ Tegeta Salasala katika maeneo ya Mjimwema kuna watu wameingia katika maeneo ya bomba la gesi na kujenga upya wakati walishalipwa ili kuondoa sasa tumewawekea alama ya ’ X ‘ ili kubomolewa na hivi karibuni watabomolewa,” alisema.
Loading...
BLOG RAFIKI
-
-
Burhan awekewa vikwazo na Marekani14 hours ago
-
-
-
-
RUZUKU YA NISHATI SAFI KUWANUFAISHA WANANCHI22 hours ago
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
Post a Comment