Saa chache baada ya kifo cha bondia mwenye makeke na vituko vingi nje ya ulingo, Thomas Mashali, baba mzazi wa bondia huyo, Christopher Malifedha amefunguka na kueleza namna alivyoletewa taarifa za kifo cha mwanaye.
Mashali anatarajiwa kuzikwa leo na baba yake alisema, wanasubiri taarifa za polisi kwanza ndipo wataamua kama watamzika Dar es Salaam au watasafirisha kumpeleka Songwe, kijijini kwao.
“Walikuja hapa (Tandale Mtogole) watu wanne saa 9.00 usiku, walipiga kelele na kugonga mlango kwa fujo wakitaka niwafungulie, nilikataa na kuwasikiliza dirishani, awali nilihisi ni polisi, walikuwa wamevaa mavazi kama ya mgambo, kati yao mmoja alikuwa na rasta na mwingine alikuwa amebeba begi mgongoni.
“Niliwataka waseme shida yao, kwani niliwaambia siwezi kuwafungulia usiku ule, kwa kweli walionekana kuwa na wasiwasi, mmoja aliniambia Mashali (Thomas) kapigwa na kapasuliwa kichwa yuko Hospitali ya Sinza,” alisema baba wa Mashali.
Loading...
Post a Comment