Loading...
RC Makonda ampigia simu Rais Magufuli mkutanoni ... Haya hapa mazungumzo yao
RC Makonda leo akiwa Ubungo ktk mwendelezo wa mikutano yake ya kusikiliza kero za wananchi. Wananchi wa Kimara waliuliza kuhusu bomoa bomoa Kimara bila kulipwa fikia.
RC Makonda wakati anafafanua aliamua kupiga simu direct kwa Mhe Rais Magufuli ambaye alipokea na kuanza kuongea kwa kutoa ufafanuzi wa kina kupitia loud speaker ya simu ya RC Makonda ambayo iliunganishwa vipaza sauti watu wote waliokuwepo wakisikiliza.
Baada ya ufafanuzi mrefu Mhe JPM aligusia kuhusu nyumba zilizoko ktk road reserve na kusema hata jengo la Tanesco kama liko ktk eneo husika litavunjwa.
Amesema serikali imepata pesa tayari kujenga interchange ya ghorofa 2/3 ya aina yake.
Mhe Rais JPM amempongeza RC Makonda na kumtaka aendelee kutatua kero za wananchi na ingependeza RC'S wengine wangeiga utaratibu huu.
Maana kero nyingi za wananchi hazijipati majibu kwa wakati kufanya hivyo itapunguza malalamiko mengi.
Mtindo huu wa mawasiliano baina ya RC na Mhe Rais umeamsha hisia chanya kwa wananchi kiasi Mhe JPM alivyomaliza kuongea wananchi walilipuka kwa Shangwe kubwa sana.
*Hongera sana serikali ya awamu ya tano.
Imeandaliwa na Tembe Nyaburi
BLOG RAFIKI
-
-
Kwa Undani4 hours ago
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
Post a Comment