Loading...
Mgombea Ubunge wa CUF ahamia CCM
Aliyekuwa Mgombea wa CUF Jimbo la Sumve,Kwimba,Mwanza Ndg Richard Ntunduru Mchele amerejea CCM leo tarehe 17/12/2016.
Viongozi na Wanachama wa Tawi la Mwangika, wamempokea Ndg Richard Ntunduru Mchele baada ya kukabidhi Kadi na Sare zake zote alizotumia Wakati wa Kampeni mbele ya Halmashauri Kuu ya Tawi na baadaye kwenye Mkutano Mkuu wa Tawi.
Aliwaeleza viongozi na Wanaccm wote kuwa, yeye ni Sawa na Mwanampotevu yule aliyetolewa Mfano kwenye Biblia sasa amerejea Nyumbani kuijenga CCM.
Baada ya kupokelewa aliahidi kuhakikisha ofisi ya CCM Tawi inajengwa kwa kiwango kinachopendeza maana imechakaa.
Zaidi aliwaahidi ushirikiano ule ule aliokuwa akiutoa awali kwa Wananchi wote utaongezeka zaidi, kwa lengo la kuisaidia Serikali ya awamu ya tano, kutekeleza Ilani ya CCM.
Mwisho aliwaomba Wanaccm wote, kuendelea kujitolea nguvu kazi zao kwenye swala la maendeleo pindi viongozi wao wanapowahitaji kufanya hivyo.
Sumve na Maendeleo!
Post a Comment