Aliyekuwa mgombea urais wa kike wa kwanza Tanzania kwenye Uchaguzi mkuu wa 2005 kupitia chama cha APPT-Maendeleo, Dr. Anna Claudia Senkoro amefariki dunia nyumbani kwake Tabata Segerea jijini Dar es salaam .
Taarifa za awali zinaeleza kuwa Marehemu Anna aliugua ghafla jana usiku na kukimbizwa hospitali kabla ya mauti kumkuta. Mwili wa Marehemu Umehifadhiwa kwenye hospitali ya Taifa Muhimbili kusubiri taratibu za mazishi.
Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahali pema peponi.
Loading...
Post a Comment