Loading...
CCM yakomba wanachama na viongozi wa Chadema 200
Akizungumza baada ya kuwapokea wanachama hao jana, Mbunge wa Bumbuli, January Makamba alisema uamuzi wao unatokana na CCM kutekeleza ahadi nyingi za maendeleo.
Bumbuli. Wanachama 200 wakiwamo viongozi wa Chadema katika Kitongoji cha Kwemghogho wilayani hapa wamekihama chama hicho na kujiunga na CCM .
Akizungumza baada ya kuwapokea wanachama hao jana, Mbunge wa Bumbuli, January Makamba alisema uamuzi wao unatokana na CCM kutekeleza ahadi nyingi za maendeleo.
Makamba alisema CCM imefanya mengi hivyo haoni ajabu kuwapokea wanachama kutoka vyama vingine vya siasa.
Alisema chama hicho kina kazi kubwa ya kuleta maendeleo ambayo yanahitaji umoja na mshikamano na siyo migogoro, fitina na majungu.
Makamba alisema moja ya mambo yanayochangia kurudisha nyuma maendeleo ni baadhi ya watu kukaa vijiweni na kurushiana maneno, lakini kwa wana-CCM muda huo sasa haupo.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema wa Kitongoji cha Kwemghogho, Shabani Kahema aliwahamasisha vijana kujiunga na CCM kwa kuwa ilani yake inatekelezeka kwa wakati.
BLOG RAFIKI
-
-
-
-
-
-
THBUB YACHUNGUZA MAUAJI YA KIUNGONI, PEMBA20 hours ago
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
Post a Comment