Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Mil 4.7 zachotwa Karatu



MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Karatu, Waziri Moris, amemuagiza mkaguzi wa ndani wa halmashauri hiyo, Hassan Juma, kufanya ukaguzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Kambi ya Simba, kata ya Mbulumbulu, wilayani humo, kufuatia tuhuma za ubadhilifu wa Sh. milioni 4.7.

Kufuatia ubadhilifu huo, Moris amemsimamisha kazi Mhasibu wa mradi huo, Selestine Dafii, ili kupisha ukaguzi huo ambao ulianza rasmi jana na kuagiza akabidhiwe taarifa ya ukaguzi huo Januari 27, mwaka huu .

Moris alitoa agizo hilo mwishoni mwa wiki wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi wa kijiji hicho.

Wananchi hao walimuandikia barua mkurugenzi huyo kumweleza ubadhilifu huo kwa ajili ya kupata msaada wa ukaguzi kutoka ofisi yake.

Moris alisema serikali ya awamu ya tano haina mzaha na mtu au kikundi cha watu kinachofanya ubadhirifu wa mali ya umma kwa ajili ya maslahi yake binafsi.

“Mkaguzi wa ndani ataanza ukaguzi wa mradi huo wa maji Januari 23, mwaka huu kwa siku nne na Januari 27 unikabidhi taarifa hiyo ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa mara moja kwa wale wote watakaobainika kuhusika kutafuna fedha za maji,.”

Alisema licha kuchukuliwa hatua atavunja kamati nzima ya maji ili wanakijiji wachague kamati nyingine ambayo itazingatia kanuni na sheria.

“Haingii akilini mradi wa maji una akaunti benki halafu mtu anakusanya fedha na kukaa nazo nyumbani kwake kama mali yake, lakini pia mwenyekiti wa kamati kushindwa kuitisha mkutano mkuu wa kijiji kama inavyoelekezwa kuwa kila baada ya miezi mitatu mapato na matumizi yasomwe kwenye mkutano mkuu. Kushindwa kufanya hivyo ni kosa kisheria,” alisema.

Kupitia mkutano huo, mkurugenzi huyo mtendaji wa halmashauri alisema baada ya ukaguzi huo kumalizika utafuata ukaguzi wa mapato ya mradi wa shamba la kijiji lenye ukubwa wa ekari 125, mradi wa trekta mbili, mradi wa kuuza moram na mradi wa ghala la kuhifadhia mazao.

Awali, wananchi hao walimlalamika kuwa kijiji chao kina mapato mengi lakini hakuna mapato na matumizi yanayosomwa kwa wakati katika mkutano mkuu na viongozi wa kijiji hicho.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top