SERIKALI imerejesha asilimia 49 ilizokuwa inazimiliki kwenye Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), ambazo baada ya shirika hilo kubinafsishwa kwa kampuni binafsi ya Simon Group kulizuka utata zilipo hisa hizo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene alimweleza Rais John Magufuli kuwa baada ya kuwa amewaagiza kufuatilia uuzwaji wa UDA, walifanya kazi hiyo kikamilifu na kufanikiwa kurejesha asilimia 49 za serikali.
“Tulifanya kazi chini ya uongozi wa Waziri Mkuu, tukafanikiwa kurejesha asilimia 49 ambazo kwa kweli zilikuwa hazijulikani ziliko, lakini hisa asilimia 49 za jiji hizi tayari tulibaini zilishauzwa kwa Kampuni ya Simon Group,” alisema Simbachawene.
Alisema walibaini pia kuwa baada ya kuuziana, baadaye walishitakiana wenyewe kwa wenyewe, hivyo wakafanikiwa kuhakikisha serikali inabaki na asilimia zake 49 kwenye UDA ambayo sasa inafahamika kama UDA RT, ambayo ndio wanaoendesha Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka.
Aliongeza kuwa baada ya kuuza hisa hizo, Halmashauri ya Jiji hatimaye ililipwa Sh bilioni 5.8 na mwekezaji huyo, lakini halmashauri ya jiji na manispaa, wanavutana juu ya matumizi ya fedha hizo.
“Wanabishana wengine wataka kila manispaa ipewe mgawo, wengine wanataka wajenge vituo vitatu ya mabasi ya mikoani, lakini hawajapata muafaka wanaendelea kubishana...haya ni majungu tu nimeamua kuyasema hapa, lakini wakishindwa tutaomba mheshimiwa Rais utoe maelekezo mengine juu ya namna ya kutumia fedha hizo,” alisema Simbachawene.
Aliongeza kuwa iwapo halmashauri ya jiji, itakubaliana na mawazo ya kujenga stendi tatu kwa ajili ya mabasi ya mikoani ya Kongowe, Mbezi na nyingine kwa ajili ya mabasi yanayotoka mikoa ya kaskazini ni wazi kuwa watakuwa wamebuni miradi mizuri yenye manufaa kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam.
Pia Simbachawene alisema DART wamekuja na mpango wa kujenga jengo lao, jambo ambalo yeye amewakatalia, kwa kuwa kufanya hivyo kuvunja fedha za mradi. Alisema amewakatalia kwa sababu serikali inahamia Dodoma na wao wanaweza kupata jengo moja kwa ajili ya kuendeshea shughuli zao.
Akizungumzia kuhusu hoja hiyo, Rais Magufuli ametoa siku tano kwa viongozi wa jiji hilo, wawe wameamua watazitumia fedha hizo kwa miradi gani.
“Nataka waje waniambie watazitumia fedha hizo kwa jambo lipi, wakishindwa sisi tutawasaidia kuwapangia. Ila nataka wasigawane, badala yake wazielekeze kwenye miradi yenye manufaa kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam,” alisema Rais Magufuli.
Akizungumzia Kampuni ya Simon Group, Rais Magufuli alisema kwamba alipanga kuitumbua kampuni hiyo, lakini bahati nzuri imelipa deni hilo.
Alisema deni hilo ndio ulikuwa mtego wake aliokuwa ameutega, kama ingeshindwa kulipa deni lake la ununuzi wa hisa za Jiji la Dar es Salaam. Alisema kwa kweli Simon Group wameonesha uwezo wa kuendesha mradi huo, na hivyo mpango wake wa kuitumbua ameufut
Alfajiri
3 hours ago
Post a Comment