Loading...
Alichokisema Rais Magufuli juu ya vita dhidi ya madawa ya kulevya
HOTUBA YA RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI
Vita ya dawa za kulevya haina cha umaarufu, haijalishi ni mtoto wa nani anahusika, hata kama ni mke wangu mkamateni- Rais Dkt @MagufuliJP
Kuna mfanyabiashara maarufu wa dawa za kulevya alikamatwa mkoani Lindi lakini sijawahi kusikia amefikishwa mahakamani- Rais @MagufuliJP
Niwepatia hii boti kusudi mkalinde huko baharini panapopitishwa magendo na dawa za kulevya nendeni mkafanye kazi. Rais Dkt @MagufuliJP
'Naagiza vyombo vyote vinavyohusika, kufanya kazi zenu, hii kazi si ya Makonda ni ya Watanzania wote, shika yoyote peleka mahakamani'-JPM
Nataka wafungwa wawe wanafanyakazi, ukiwafunga tu na kuwapa chakula ndio sababu wanarudia makosa kila siku wakitoka- Rais Dkt JPM
"Makonda mshutumiwa wa madawa ya kulevya ikiwezekana muweke hata kwenye magazeti yote na hadi kwenye vipeperushi. BANDIKA TU!" -JPM
'Madhara ya dawa za kulevya kwa taifa letu sasa hivi yamefikia mahali pabaya, haiwezekani watu wanauza kama njugu'-JPM #IKULU
Post a Comment