MKUU wa Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro, Aaron Mbogho ameagiza watumishi watatu wa halmashauri hiyo akiwamo Mweka Hazina, Subilaga Kapange kuwekwa rumande kwa saa zisizozidi 48 kwa madai ya kwenda kinyume cha taratibu za kazi.
Pamoja na Mweka Hazina, watumishi wengine waliowekwa ndani ni maofisa ardhi wawili, ambao majina yao hayakupatikana mara moja ambao wote kwa pamoja wanatakiwa kutumikia adhabu hiyo.
Akizungumza kwa simu, Mbogho alisema alitoa uamuzi huo jana saa tano asubuhi baada ya kujiridhisha makosa waliyofanya watumishi hao.
“Ni kweli nimeagiza watumishi hao wawekwe ndani, na nimesimamia mwenyewe hadi nilipoona wanakuja kuchukuliwa na polisi ili kuwekwa ndani...sababu za uamuzi huo siyo lazima wewe uzijue, cha msingi nimethibitisha tukio,” alieleza mkuu wa wilaya.
Aliongeza kuwa, “Zipo mamlaka ambazo mimi napaswa kuzipa taarifa juu ya uamuzi niliochukua na sababu yake...wewe elewa kwamba ninayo mamlaka ya kufanya hivyo, huyo mtu aliyekueleza, akupe na sababu za mimi kufanya hivyo.”
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Golden Mgonzo alithibitisha kukamatwa kwa watumishi hao, lakini akataka sababu za kukamatwa kwao aulizwe DC.
“Ni kweli mkuu wa wilaya ametoa amri hiyo, lakini siwezi kukutajia hayo majina kwani muda huu nipo katika kikao, ebu muulize mkuu wa wilaya mwenyewe,” alisema.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Theresia Msuya alisema hana taarifa za kukamatwa huko.
“Mimi sina taarifa hizo, wewe ndiye unayeniambia, leo nipo nyumbani nimepumzika. Jana (juzi) tumetoka hapo katika kikao cha baraza cha bajeti, ebu waulize watu wengine juu ya tukio hilo,” alisema Msuya.
Loading...
BLOG RAFIKI
-
-
-
-
-
THBUB YACHUNGUZA MAUAJI YA KIUNGONI, PEMBA15 hours ago
-
THBUB YACHUNGUZA MAUAJI YA KIUNGONI, PEMBA15 hours ago
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
Post a Comment