Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Mkandarasi Ujenzi 'fly over' Tazara abanwa


WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, amemtaka Mkandarasi wa kampuni ya ujenzi ya Sumitomo Mitsui anayejenga barabara ya juu (fly over) ya Tazara, kuongeza kasi ya ujenzi huo.

Prof. Mbarawa alitoa agizo hilo jijini Dar es Salaam juzi muda mfupi baada ya kumaliza kutembelea mradi huo uliozinduliwa Desemba mosi, mwaka juzi na kufurahishwa na kasi ya ujenzi inayoendelea.

Ziara hiyo aliifanya akiwa amefuatana na Balozi wa China nchini Tanzania, Masaharu Yoshida.

Licha ya kupongeza hatua ya ujenzi ilipofikia hivi sasa ya kukamilika kwa asilimia 25.3 kati ya 25.8, alimtaka mkandarasi huyo kuongeza kasi zaidi ya ujenzi huku akizingatia ubora na viwango vilivyowekwa.

“Kama mnakumbuka, Rais John Magufuli wakati akizindua mradi huu aliomba muda wa ujenzi ambao ni miezi 35, angalau upungue, nimefurahishwa na kasi yenu hakikisheni miezi ya ujenzi wa mradi inapungua zaidi ili kuwawezesha wananchi na wadau wengine kunufaika na fursa hii itakapokamilika, ”alisisitiza Mbarawa.

Pia alimtaka mkandarasi kuhakikisha ujenzi huo unatekelezwa kwa viwango vilivyowekwa ili viendane na fedha ambazo ni zaidi ya Sh. bilioni 96.5 zilizotengwa kutekeleza mradi huo unaotarajiwa kukamilika Oktoba, mwakani.

Aidha, aliwataka wafanyakazi wote katika mradi huo kufanya kazi kwa bidii na uaminifu kwa kuwa serikali ina mpango mwingine wa kujenga fly-over kama hiyo itakayowawezesha kupata fursa ya ajira.

Naye Balozi Yoshida alimhakikisha Waziri Mbarawa kuwa ujenzi wa mradi huo utamalizika kwa wakati na kwa viwango vilivyokusudiwa na hivyo kuondoa changamoto ya msongamano katika barabara ya Nyerere na Mandela.

Mkurugenzi wa Miradi kutoka Wakala wa Barabara nchini (Tanroads), Mhandisi Chrispianus Ako, alisema kati ya nguzo 66 zinazohitajika kwenye awamu ya kwanza ya ujenzi huo, tayari 43 zimeshasimikwa ardhini, hali itayoufanya ujenzi huo kwenda kwa kasi.

Alisema kazi ambazo zimefanyika kutoka Septemba 30, mwaka jana hadi jana ni ujenzi wa barabara ya Kusini mwa mradi huo, ambayo ikikamilika itatumiwa na magari ili ujenzi wa daraja hilo uendelee.

“Mheshimiwa Waziri Mbarawa, kutoka Septemba, mwaka jana ulivyotembelea mradi na kukuta maendeleo ya ujenzi ambayo yalikuwa kwa asilimia 13, kwa sasa tumepiga hatua nyingine na ujenzi wa mradi kwa awamu hii umefikia asilimia 25,” alisema.

Alisema kutoka wakati huo kazi ambazo zilikuwa zikifanyika ni ujenzi wa barabara upande wa Kusini, kusafisha eneo la mradi,
kujenga tabaka la kwanza ambapo hadi sasa tayari kumeshawekwa lami.

Alisema kazi iliyobaki ni kuweka tabaka la pili juu.

Pia alisema katika ujenzi wa daraja, wameanza kusimika nguzo zinazoanzia mita tisa hadi 13.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top