Loading...
Mke wa Marehemu Komba amwangukia Rais Magufuli .... Aidai CCM Tsh. Mil 75
Ikiwa Leo ni miaka miwili tangu kifo cha aliyekuwa kada maarufu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Captain John Komba, Mkewe bi Salome Komba ameibuka na kumuomba mwenyekiti wa Chama hicho Rais Dk John Magufuli amsaidie ili aweze kulipwa 'Mafao' na 'Stahiki' za Mumewe.
Akiongea kupitia kipindi cha Maisha Mseto cha Times Fm mapema Leo asubuhi, Bi Salome amedai kuwa wanaidai CCM mafao ya Shilingi Milioni 75 kama jasho la Mumewe alivyokitumikia Chama ila mpaka sasa wamelipwa Shilingi Milioni 4 na laki 5 pekee.
"Namuomba Mwenyekiti wa CCM anisaidie niweze kupata mafao ya Marehemu, alikuwa anaipenda sana CCM na mpaka anafariki alikuwa ameanza kuwahamasisha Wasanii kuhusiana na kampeni" Alisema.
"Niliongea na katibu Mkuu, nadai kama Milioni 75 ila nmepewa Milioni 4 na laki 5 tu na ni Mwaka wa Pili sasa hivi, hivyo naomba nisaidiwe nipate Jasho lake ni haki Yake kwa jinsi alivyojitoa kwenye Chama, na amefariki akiwa ndani ya CCM" Aliongeza Bi Salome.
Katika hatua nyingine Mjane huyo amesema kuwa, ameamua kugawa bure nakala za vitabu vinavyoelezea Maisha ya Marehemu Komba kwa sababu Watanzania hawana utaratibu wa kujisomea.
Post a Comment