Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

RC Makonda awaangukia viongozi wa dini

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewaomba viongozi wa Dini kuendelea kuamrisha mema na kukataza mabaya, kwani kufanya hivyo kunaipunguzia serikali mzigo.

RC Makonda ameyasema hayo alipokuwa anafungua semina kwa Walimu wanaosomesha Qur-an Tanzania (JUWAQUTA) na kusisitiza kuwa viongozi wa dini wakiwafundisha mema waumini ambao ndiyo wananchi, Taifa halitakuwa na wahalifu au matukio ya wizi, ujambazi, utumiaji wa dawa za kulevya na ufanyaji wa biashara hiyo, jambo ambalo litaipunguzia gharama serikali ya kuwahudumia waathirika kwa kuwapa vidonge vya Methadone, na serikali haitatumia nguvu kubwa kujenga magereza kwa ajili ya wanaokiuka sheria na taratibu za nchi.

Na kusisitiza kuwa serikali itaendelea kuwaunga mkono viongozi wa dini kwani wanamchango mkubwa kwenye maendeleo ya Taifa hili.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa JUWAQUTA ambaye pia ni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum amesema kuwa lengo la semina hiyo ni kuwaelimisha walimu hao juu ya kuunga mkono kauli mbiu ya HAPA KAZI TU ya serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli kwani kufanya kazi ni agizo kwa mujibu wa dini hiyo ya kiislamu ambapo waumini wake wameambiwa wafanya kazi za halali ili wapate ridhiki halali na siyo vinginevyo.

Huku akifafanua kuwa hata manabii walikuwa wakifanya kazi hivyo ni vyema kama viongozi kufuata nyayo hizio na kuwaamrisha wengine kufuata utaratibu huo.
.Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza katika unafunguzi semina ya Walimu wanaosomesha Qur-an Tanzania (JUWAQUTA) leo jijini Dar es Salaam.
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum akizungumza katika unafunguzi semina ya Walimu wanaosomesha Qur-an Tanzania (JUWAQUTA) leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akiombewa dua na viongozi dini, leo jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka,Glob ya Jamii. 

Picha ya Pamoja
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top