Loading...
Home » Unlabelled » SAKATA DAWA ZA KULEVYA .... Hatimaye Mbowe kaachiwa huru ... Hii hapa Taarifa waliyoitoa Chadema
SAKATA DAWA ZA KULEVYA .... Hatimaye Mbowe kaachiwa huru ... Hii hapa Taarifa waliyoitoa Chadema
Kama tulivyowajuza kwamba iwapo itatokea jambo lolote la umuhimu kujuzana kabla ya asubuhi tutafanya hivyo, tunapenda kuwatangazia wanachama wetu,wadau,wapenzi, na wapenda haki,amani na demokrasia ya kwamba Mwenyekiti Freeman Mbowe ameachiwa huru punde tu mnamo majira ya SAA saba na robo usiku huu.
Tunawashukuri wote kwa sala,maombi na subira na hivyo kuhitimisha salama SAA KUMI za Mwenyekiti wetu kuwa chini ya Jeshi la Polisi nchini katika kituo kikuu cha Polisi jijini Dar es salaam.
Taarifa za ziada juu ya jambo hili zitatolewa kesho.
Salum Mwalim
Naibu Katibu Mkuu
Chadema
Post a Comment