Zanzibar.Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, wameshauri kuwekwa adhabu kali kwa atakayejitangazia ushindi katika Uchaguzi Mkuu.
Kauli ya wawakilishi hao imekuja baada ya aliyekuwa mgombea urais wa Zanzibar kupitia CUF katika Uchaguzi Mkuu uliopita, Maalim Seif Sharif Hamad kujitangaza mshindi wa uchaguzi huo.
Wajumbe hao walishauri adhabu ya kifungo cha maisha jela kwa mgombea wa nafasi ya kisiasa atakayejitangazia ushindi, kabla ya matokeo kutangazwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).
Wakichangia Muswada wa Sheria wa Kufuta Sheria ya Tume ya mwaka 1992 na kutunga sheria ya kuanzisha Ofisi ya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), majukumu na uwezo, wajumbe hao walisema muswada huo unapaswa kutekelezwa haraka.
Katika kikao kilichoendelea jana Chukwani nje kidogo ya mji wa Unguja, Mwakilishi wa Jimbo la Kwahani, Ali Salim amesema adhabu iliyomo ndani ya muswada huo faini ya Sh500,000 au Sh1 milioni ni ndogo ukilinganisha na kosa la kujitangaza mshindi.
Loading...
Post a Comment