Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

SAKATA MADAWA YA KULEVYA .... Mchungaji Gwajima naye atema cheche




KUTOKA KWA MCHUNGAJI GWAJIMA LEO 09.02.2017


Gwajima:- Namuomba Rais ambadilishie Kazi Makonda,  hii ya Ukuu wa Mkoa kutawala na kuongoza hata watu usiowapenda imemshinda.  Sisemi amfukuze hapana nasema ambadilishie Kazi.

Gwajima : Makonda ana chuki na wivu na mimi

Gwajima : alikasirika hata niliposhuka na helkopta yangu siku ya mechi ya viongozi wa dini na wabunge dodoma.

Gwajima : nilichelewa kidogo nikaamua kupanda helkopta yangu mpaka uwanjani kabisa.

Gwajima : mimi nilicheza namba kumi  Makonda namba tisa,  jicho alilokuwa ananiangalia ni la chuki mpaka nikawa nashangaa.

Gwajima : hii hapa picha niko na Makonda,  naibu spika na viongozi wengine tukichangia ujenzi wa taifa mbona hajanikamata hapa kama ninauza unga? .

Gwajima : Makonda alikuja kanisani kwangu na marehemu sitta na akapanda mazabauni je hakujua kama nauza unga? .

Gwajima : hili ni shambulio kwa kanisa sio kwa Gwajima

Gwajima : hili ni shambulio kwa wote walio okoka tuonekane hatufai

Gwajima : hili ni shambulio kwa maaskofu wote na wachungaji wote

Gwajima : kwa sababu Gwajima ana kanisa kubwa

Gwajima : kwa sababu Gwajima ana waumini zaidi ya elf sabini kanisani kwake na makanisa zaidi ya 400 nchi nzima.

Gwajima : nilikuwa mkali Sana kwa  serikali ya awamu ya nne na kikwete

Gwajima : nilikemea sana kupotea kwa ndovu kila siku

Gwajima; Makonda anafanya hivi kwa maslahi ya Nani? .

Gwajima : Makonda anafanya hivi kufurahisha serikali iliyopita ionekana nimekomolewa.

Gwajima : Hili ni shambulio kwa Ukristo.  Rais wangu mpendwa mbadilishie Kazi Makonda.

Gwajima : Makonda hajatumwa na Rais kufanya anayoyafanya

Gwajima : mimi namfahamu vizuri Rais,  hawezi kumtuma Makonda kufanya hivi.

Gwajima : Makonda atavuka mipaka sasa,  atakemea Polisi,  atakemea jeshi, atakemea wabunge

Gwajima : Makonda atakemea mpaka waziri mkuu.

Gwajima;  wenzetu wabunge wameungana kutumia sheria na kanuni zao watamuhoji.

Gwajima : sisi raia wa kawaida tusio na sheria wala kanuni za kututetea tutashtaki wapi? .

Gwajima: Nakumbuka Kuna siku Makonda alikuwa anahutubia, akamwambia Waziri mkuu eti nlipiga marufuku shisha lakini imerudi, hawa wavuta shisha waliniletea Milion 5 nikakataa akasema lakini naamini kamanda Siro hizi milioni tano tano zimepita kwao. Makonda alidiliki kumtuhumu Waziri MKuu eti Karudisha Shisha!?. DC Makonda ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar, kwanini hakuisemea kwenye Vikao, Kwanini alisubiri Media?

Gwajima: Safari hii kamfikia kiongozi wa Kiroho, huu ni unafiki sana. Huweze kumuita rafiki yako kaka yako namna hii.

Gwajima: Sasa leo nataka niwambie kwanini Makonda anafanya hivi;

1. Nataka niwambie, Rais hajamtuma Makonda atutuhumu sisi

2. System za Serikali zimeparalyse kwa sababu watendaji wa Serikali na Mawaziri wanamuona Makonda ni Mkono wa kiume wa Rais. Wanafikiri labda kwakuwa Makonda ni Msukuma basi atakuwa anatumwa na rais, Rais hawezi kufanya hivyo. Mawaziri wamekosa neno wamekaa Kimya.

Gwajima: Nani anatakiwa kuniita mimi kama Askofu Mkuu Polisi? Ni Polisi sio Makonda. Makonda anajiona kama Mkuu wa Wakuu wa Mikoa yote na Mawaziri wote.

Gwajima: Sio desturi ya rais hata kidogo eti awatenge Mawaziri wake eti aongee na Makonda. Rais alikuwa anampongeza makonda kwa sababu kafanya Vizuri. Makonda anaujasiri na anajituma hivyo rais kumpongeza ni halali. Makonda anaweza kuwa Kiongozi Muu siku zijazo kama akiondoa baadhi ya Hitilafu.

Gwajima: Makonda angeweza kunipigia simu au Kuwagiza Polisi wakaniletea samasi au kuniita.

Gwajima: Nia ya Makonda ni kutaka jina la Gwajima liharibike. Kama Gwajima hafanyi na hajihusishi na Madawa ya kulevya watu wa Usalama wanajua. Nmefanya hii kazi ya Uchungaji kwa Miaka 20.

Gwajima: Si kweli kwamba makonda anatumwa na Rais, rais ana tabia ya kupongeza saa nyingine anapiga simu Clouds kupongeza pale wanapofanya Vizuri.

Gwajima: Sisi tunamuunga mkono Mheshimiwa rais hata kama kwenye uchaguzi hatujamuunga mkono, Lakini kwa kuwa amechaguliwa yeye tunamuunga mkono

Gwajima: Naamin Makonda hajajificha kwenye "Usukuma" wake.

Gwajima: Namuomba rais amkanye Makonda. Chuki zake binafsi za mtu mmoja mmoja asiziingize kwenye system ya Serikali, ni hatari sana

Gwajima: Makonda ni Mchapakazi lakini Mambo ya Utawala hawezi, namuomba rais amtafutie kazi nyingine, nashauri umtafutie kazi nyingine, sio umfukuze.

Gwajima: Chini yangu kuna Maaskofu 125. Kesho wataogopa nao watasemwa

Gwajima: Kuna siku Paul Makonda, Sitta na Mwakyembe walikuja kanisani kwangu hata CD ninazo na alihutubia hapa kwenye Madhabahu akinisifia sana, Leo ni kitu gani kimemfanya anichafue?

Gwajima: Je ikiwa Gwajima hahusiki, itakuwaje?

Mimi nlikuwa makali sana juu ya utawala wa awamu ya nne. Miaka kwa miaka Tembo walikuwa wanakufa.

Nani anamtumia Makonda?

Makonda ana nia ovu juu yangu na juu ya Wakristo. Anataka kuwaaminisha watu kwamba wokovu haupo.

Mimi nataka kununua ndege nyingine ili nianzishe chuo cha ndege, mbona sipongezwi kwa hilo?

Jambo hili alilofanya si sawa na si sahihi.

Wabunge wamepiga kelele juu ya jambo hili, sisi wananchi tusio na sehemu ya kuongea tufanyeje?

Namfahamu rais magufuli, hawezi kumpendelea kwa kuwa ni mtu wa kwao (msukuma). Rais anawapenda watu wote anawapenda Mawaziri wote. Naamin rais hajamtuma Makonda.

Nguvu katika mikono isiyo sahihi ni hatari sana.

Mimi Makonda, kamanda Sirro Spika wa Bunge si angenikamata hapo?

Kuna watu walikuwa wanauza madawa ya kulevya, katika uongozi huu wale walikuwa wanauza madawa ya kulevya wamebadili majina na wanafanya biashara nyingine.

Chanzo: Jambi la Habari
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top