Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Serikali kujenga kiwanda cha kutengeneza simu


 Serikali imesema inalenga kuanzisha kiwanda cha kutengeneza simu hapa nchini ili kuwalinda watumiaji.


Akijibu bungeni, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amesema kwa sasa wanawashukuru watendaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kugundua simu feki kwa sababu zina madhara kwa binadamu.


Mwijage alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Aida Khenani aliyeitaka Serikali kuwalipa fidia wananchi walioathirika na kufungwa kwa simu feki kwa sababu watendaji wake hawakuwa makini wakaruhusu ziingizwe nchini na kulipiwa kodi.


“Serikali ina mpango gani wa kuwalipa watu walioathirika na kuzimwa kwa simu feki uliotokana na uzembe wa watendaji?” amehoji.


Akijibu swali hilo, Mwijage amesema Serikali inadhibiti uingizwaji wa bidhaa hizo kwa kuimarisha ukaguzi, kuendelea kuajiri wataalamu zaidi na kufungua vituo vya ukaguzi wa ubora wa bidhaa katika mipaka zinakopitishwa kutoka nchi nyingine.


Pia, amesema Serikali hufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwenye njia za kuingizia bidhaa ikiwamo Bandari ya Dar es Salaam, Tanga na Mtwara, viwanja vya ndege vya Julius Nyerere na Kilimanjaro na mipaka inayopitishiwa bidhaa kutoka nje ya nchi.



“Serikali itaendelea kuwachukulia hatua wale wote watakaohusika na uingizaji wa bidhaa bandia ikiwa ni pamoja na kuziteketeza  au kuzirejesha zilikotoka,” amesema Mwijage.

Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top