Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,kikanda na kimataifa imekiri kupokea taarifa ya kukamatwa na kufukuzwa kwa zaidi ya Raia wa Kitanzania mia moja thelathini na wawili waliokuwa wakiishi katika mji wa Monte Puez nchini Msumbiji na kwamba Ubalozi wa Tanzania nchini humo unaendelea kufanya mazungumzo na Serikali ya nchi hiyo ili kuhakikisha Usalama wao na mali zao.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari Naibu waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki,kikanda na kimataifa Dr Suzan Kolimba ametaja sababu iliyosababisha hatua ya kufukuzwa kuwa ni kufuatia operesheni maalum inayoendelea nchi Msumbiji ya kuwakamata na kuwarudisha Raia wa kigeni wanaoishi katika mji huo bila kufuata Sheria za Uhamiaji.
Aidha amesema kuwa kuanzia zoezi hilo lilipoanza zaidi ya raia wapatao 132 wamesharudishwa nchini ambapo February 11 walirejeshwa watanzania hamsini na wanane, February 14 raia ishirini na wanne huku pia kukiwepo taarifa ya kerejeshwa watanzania 50 kwa leo February 15. Kwa mujibu wa Naibu Waziri huyo inakadiriwa Watanzania zaidi ya 3000 wanaishi na kufanya Shughuli za kiuchumi na kijamii katika Mji wa Monte Puez.
Kufuatia hali hiyo Serikali imetoa tamko linalowataka Watanzania wote wanaotoka na kwenda nje ya nchi mbalimbali ndani na nje ya bara la Afrika Kufuata Sheria na utaratibu wa nchi wanazoishi ama wanazofanyia shughuli zao za kiuchumi na kijamii ili kuepukana na usumbufu wa kukamatwa na kufukuzwa .
Loading...
Home » Unlabelled » Serikali yatoa tamko kukamatwa, kuteswa na kufukuzwa kwa Watanzania nchini Msumbiji
Post a Comment