Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imekusanya Sh trilioni 8.41 kuanzia Julai mwaka jana hadi Januari mwaka huu.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Richard Kayombo, inaonesha makusanyo ya Januari mwaka huu ni Sh trilioni 1.14.
Kayombo alisema pamoja na juhudi za kukusanya kodi mbalimbali, hivi sasa wameelekeza nguvu katika kukusanya kodi ya majengo kwa kutoa ankara kwa wamiliki wa majengo katika mikoa mbalimbali.
“Wamiliki wa majengo wanakumbushwa kwamba kodi ya majengo inakusanywa na TRA kuanzia Julai mwaka jana, hivyo tunawaomba watoe ushirikiano kwa kulipia ankara zao kwa wakati,” alisema Kayombo.
Kuhusu zoezi la uhakiki wa Namba ya Mlipakodi (TIN), alisema kuna mafanikio makubwa na kwamba wananchi wa mikoa ya Arusha, Mwanza, Kilimanjaro, Dodoma, Mbeya, Morogoro, Tanga na Pwani waitikie wito huo mapema kuepuka usumbufu.
Post a Comment