Mirerani. Wachimbaji wa madini ya tanzanite wameunga mkono hatua ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kusitisha fedha za ruzuku kwa wachimbaji ili kuandaa utaratibu mpya utakaowezesha na wao kufaidika.
Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji wa Madini Mkoa wa Manyara (Marema), Sadick Mneney alisema mchakato wa kupatikana kwa wanufaika wa ruzuku hiyo inabidi upangwe upya kwa kuwashirikisha viongozi wa Shirikisho la Madini Tanzania (Femata) wanaotambua matatizo yanayowakabili wachimbaji.
Alisema robo ya waombaji wa ruzuku hiyo wanatoka Mji Mdogo wa Mirerani kwenye madini ya tanzanite, lakini wanashangaa hadi sasa hakuna aliyepata.
Mneney alisema wachimbaji wa tanzanite wanatakiwa kuangaliwa kwa jicho pevu, hivyo viongozi wa idara ya madini wanatakiwa kuwaeleza walipokosea ili utaratibu mpya ukifanyika wapate fedha.
Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kaskazini, Adam Juma alisema mchakato wa kuwapata wachimbaji wa kupata ruzuku unafanyika kwenye ngazi tofauti.
Juma alisema ili mchimbaji afuzu, anatakiwa kufuata vigezo ikiwamo kulipa kodi, leseni isiyodaiwa, mgodi kufanya kazi, uzalishaji na kuwa na namba ya utambulisho wa mlipa kodi
Loading...
Post a Comment