Kumbe staa wa filamu za Kibongo, Wastara Juma, aliye mama wa watoto watatu, mmoja kati yao, alizaa na mkongwe katika Bongo Hip Hop, Msafiri Kondo ‘Solo Thang’.
Akiongea wiki hii katika kipindi cha Uhondo cha EFM, Wastara alisema mtoto wao huyo kwa sasa ana umri wa miaka 13.
“Mtoto wangu wa pili kwa sasa ana miaka 13, nimezaa na Msafiri Kondo (Solo Thang),” alisema muigizaji huyo ambaye ni mfanyabiashara.
Kwa sasa muigizaji huyo anatoka kimapenzi na msanii wa filamu Bondi Bin Sinani ambaye ni meneja anayesimamia kazi zake za filamu.
Post a Comment