Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Bashe, Malima na Msukuma wafanya fujo mkutano wa CCM .... Watiwa mbaroni

Wabunge Hussein Bashe wa Nzega Mjini na Joseph Kasheku wa Geita wakiwa na aliyewahi kuwa mbunge wa Kisarawe, Adam Malima wamehojiwa polisi na kisha kuachiwa baada ya kukamatwa kwa tuhuma za kupanga njama za kuvuruga mkutano mkuu wa CCM

Inaelezwa kuwa, wabunge hao ambao ni wajumbe wa mkutano mkuu maalum wa CCM, ambao unatarajiwa kufanyika kesho, Machi 12 mjini Dodoma walikuwa wakipanga njama za kuvuruga mkutano huo kwa kugawa pesa kwa baadhi ya wajumbe.

Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma amethibitisha kukamatwa kwa wabunge hao, kwa ajili ya mahojiano, lakini amesema kuwa baada ya mahojiano, wabunge hao wameachiwa kwa dhamana baada ya kujidhamini wao wenyewe.

"Walikuwa wanahojiwa tu lakini kwa sasa wameshaachiwa, kulikuwa na tuhuma kwamba wanagawa hela wanapanga kuvuruga mkutano wa CCM, wamejidhamini wenyewe, na upelelezi bado unaendelea ili kubaini kama ni kweli" Amesema Kamanda Mambosasa

Kuhusu endapo watu hao walikutwa na pesa, Kamanda amesema mmoja kati yao amekutwa na pesa lakini akadai kuwa ni pesa zake kwa ajili ya matumizi binafsi.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top