Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

BREAKING NEWS .... Sophia Simba aaga rasmi



Leo tar 04.03.2017 ikiwa ni uzinduzi wa Siku ya wanawake Duniani inayotarajia kufanyika tar 08.03.2017.

Mwenyekiti wa UWT Mhe.Sophia Simba alisheherekea siku hii na viongoz wa UWT Wilaya ya Temeke ambapo katika sherehe hii alianza kwa kufanya usafi hospitali ya Temeke na viongozi hao wa Temeke na kisha kutoa vifaa  mbalimbali vya misaada kama pampers,sabuni na mataulo ya watoto yaliyotolewa ktk wodi hyo ya wazazi.kisha Mwenyekiti wa Uwt mhe Sophia Simba na wajumbe hao walielekea ukumbi wa halmashauri ya wilaya hiyo ambapo pamoja na kuazimisha uzinduzi wa sherehe ya siku ya wanawake Duniani pia alitangaza kutowania kugombea nafasi yake ya uenyekiti wa Uwt Taifa katika uchaguzi unaotarajia kufanyika mapema mwezi October mwaka huu.

Mama Sophia ameshatumikia nafasi mbalimbali za uongozi wa chama na serikali ikiwemo uwaziri na ameshakuwa mbunge Kwa kipindi cha miaka 22 hadi sasa.Pia Mama Sophia Simba amekuwa mstari wa mbele kutetea haki za wanawake nchini Tanzania.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top