Loading...
CHADEMA YAPATA PIGO KUBWA MWANZA
Uongozi mzima wa chadema wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza Leo umekihama chama hicho na kujiunga na CCM, sababu ni uamuzi wa juu wa chadema kumpokea Wema Sepetu kujiunga na chadema.
Viongozi 15 wilaya ya Ilemela akiwemo Mwenyekiti wa chama hicho Damas Kimenyi, kujiunga Ccm. Wamshutumu Freeman Mbowe (Mwenyekiti Taifa Chadema) kwamba anaunga mkono matumizi ya dawa za kulevya nchini.
Makada 15 wa Chadema waliojitambulisha kuwa viongozi wa chama hicho Wilaya ya Ilemela Mkoa wa Mwanza wamehama chana hicho na kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM).
Makada hao wakiongozwa na Damas Kimenyi aliyejitambulisha kuwa Katibu Chadema wa Wilaya hiyo walitaja kuridhishwa na utendaji wa Rais John Magufuli na mbunge wa jimbo la Ilemela, Angelina Mabula kuwa miongoni mwa sababu za kujiunga na CCM.
Wanachama hao wapya walipokelewa katika ofisi za CCM Wilaya ya Ilemela leo (Alhamisi) jioni wakati wa hafla iliyoongozwa na Mwenyekiti wa wilaya hiyo, Nelson Mesha.
Hata hivyo, Katibu Chadema Kanda ya Ziwa Victoria, Meshack Micus amesema waliohamia CCM walishavuliwa uongozi tangu Januari 18, mwaka huu wakati wa kikao cha Mkutano Mkuu wa wilaya ambacho pia kilihudhuriwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe.
“Hao ni wanachama wa kawaida na pengine wameondoka kwa hasira ya kuvuliwa madaraka baada ya Mkutano Mkuu kuunda kamati ya muda ya uongozi chini ya uenyekiti wa Warioba Wanzagi na Katibu wake Peter Kaiza,” amesema Micus.
Wengine waliojiunga na CCM ni Lukas Syrilo (Katibu wa Baraza la Vijana Bavicha), Agnes Majora (Katibu wa Baraza la Wanawake, Bawacha), Lucy Kazungu (Mwenyekiti Bawacha), na Edwine Sarung aliyejitambulisha kuwa Mweka Hazina.
Pia wamo Philipo Richard Mjumbe wa kamati tendaji wa Wilaya, Ester Ayoub Makamu Mwenyekiti wa wazee Wilaya, John Haule Mwenyekiti Bavicha, Vestina Johnson Mjumbe wa Bawacha Wilaya na Yohana Emanuel Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa wilaya.
----------------
Piga ndege wawili kwa jiwe moja, ambapo utapata OFFERS mbili za kutangaza
Mosi; Kwenye blog http://www.ndgshilatu.blogspot.com ambapo litaweka kwenye USO wa blog pamoja na kurushwa Mara kwa Mara kama post ya habari.
Pili; Kama haitoshi tangazo lako tutalitangaza pia kupitia akaunti za FaceBook na Twitter za Blog hii.
Kwa kutangaza nasi biashara ama huduma yako itawafikia zaidi ya Watazamaji 50,000+ na zaidi ya nchi 120+ wanaozitembelea Blog na akaunti hizi kila siku.
Kutokana na hii ni wazi kuwa Tangazo lako litawafikia watu wengi zaidi Duniani ndani ya muda mfupi
Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia e-mail pbuyegu2@gmail.com
Offer hii itadumu kwa muda mfupi tu ila tangazo lako litawekwa hewani kwa muda wa mwezi mzima.
Changamkia fursa hii adimu uimarishe Biashara yako.
BLOG RAFIKI
-
-
-
-
-
Alfajiri5 hours ago
-
-
-
-
-
-
Serikali yatoa kauli kuhusu Dbi ya Kariakoo9 months ago
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-



Post a Comment